Virusi vya Korona na Kristo

NINAANDIKA KITABU HIKI kidogo katika siku za mwisho za mwezi Machi 2020, tukiwa mwanzoni kabisa mwa janga hili lililokumba ulimwengu mzima lijulikanalo kama Virusi vya Korona, au “Ugonjwa wa Virusi vya Korona wa 2019” (kwa ufupi COVID-19). Virusi hivi huathiri mapafu, na visa vibaya zaidi huua kwa kusababisha msongo wa pumzi.