Tunapookolewa kwa kumwamini Yesu ni tarajio lake Yesu maana katika Injili ya Marko 16:15, Asema; “Enendeni ulimwengu mwote mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe” kwa nini? Jibu lapatikana katika Injili ya Yohana 3:16 “kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ila kila amwaminiye asipotee bali awe na uzima wa milele.”