WOTE WAAJIBIKE (MUME NA MKE)

. Mungu aliiangamiza dunia wakati wa Nuhu kwa sababu wanadamu walishindwa kukabiliana na tamaa za kuonana kwa mume na mke. Ikawa wanayafanya mapenzi kiholela holela, ikawa afadhali Wanyama wa porini. Nasoma mwanzo 6:1-2. “Ikawa wanadamu walipoanza kuzidi usoni pa nchi na wana wa kike walizaliwa kwao. 2. Wana wa Mungu waliwaona hao binti za wanadamu ya kuwa ni wazuri, wakajitwalia wake wo wote waliowachagua. Bwana wetu Yesu Kristo pia, katika Injili ya Mathayo 24:36-37, alitoa unabii akasema, “36 Walakini habari ya siku ile na saa ile hakuna aijuaye, hata malaika walio mbinguni, wala Mwana, ila Baba peke yake. 37 Kwa maana kama vile ilivyokuwa siku za Nuhu, ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.” Nyakati hizi zetu, zimekuwa zaidi ya wakati wa Nuhu. Uzinzi na usherati umezidi. Talaka na ndoa kuvunjika ni hadithi za kila siku. Mipango ya kando ni tele, nao wengi wametuacha kwa sababu ya maradhi yasiyokuwa na tiba.

sajili ya -barua pepe

Sign up for the TWR360 Newsletter

Access updates, news, Biblical teaching and inspirational messages from powerful Christian voices.

Ahsante kwa kujisajili ili kupata ujumbe kutoka TWR360Thank you for signing up to receive updates from TWR360.

Habari inayohitajika haipo