Je? Ushawaji kufikiria ingelikuwaje kuishi katika siku za Bibilia? Kutembea na wana wa Israeli jangwani, kukutana na wanaume na wanawake na watoto waliosikia kuhusu amri za Mungu kwa mara ya kwanza? Kuzigusa pazia maridadi za hema la kukutania na kumwabudu Mungu, jinsi walivyofanya zamani? Hizi ni hadithi hai za Bibilia na zinasimulia kuhusu waisraeli jinsi walivyomuabudu Mungu aliyewaumba, kuwapenda na kuwaokoa.Tunaweza kumwabudu Mungu papa hapa tulipo naye ametuonyesha njia ya kupokea msamaha wa dhambi na ondoleo la aibu pia.