Yaweza kuwaje kutazama jinsi Mungu alivyowalinda watu wake na kuwapiga maadui wa Waisraeli kupitia kwa viongozi,mahakimu na wafalme? Hii ni hadithi ya mwa zo wa shujaa mkubwa wa Bibilia aitwaye Samsoni.Hata ingawa Samsoni alifanya baadhi ya maamuzi mabaya,Mungu alikuwa na mipango mikubwa katika Maisha yake na alikuwa anaenda kumtumia kuwaokoa watu wa Israeli.Mungu angali anawainua madhujaa na viongozi leo,na ana mpango wa kupendeza maishani mwako pia.