Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Amosi, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Amosi anawashutumu Waisraeli kuwa wamevunja agano lao na Mungu, na anaangazia jinsi ibada zao za sanamu zimesababisha udhalimu na kutelekezwa kwa maskini.
#BibleProject #Biblia #Amosi