Larry Alston ni Rais na Afisa mtendaji mkuu wa huduma ya “ Christ to the world”. Yeye ni mzaliwa wa Shreveport, Louisiana. Alilelewa New Orleans. Kwa sasa anaishi eneo la Longview, Texas. Yeye pamoja na mke wake wameoana kwa miaka thelathini na tatu, na wana watoto watatu waliokomaa, wakwe wawili, na wajukuu wawili kwa majina Luke aliye na umri wa miaka mitatu na Sutton aliye na mwaka mmoja. Alikiri hadharani kumuamini Yesu Kristu kama mwokozi wa maisha yake akiwa umri wa miaka kumi na mitatu. Alihitimu na shahada ya sanaa katika Chuo Kikuu cha New Orleans mnamo mwaka wa 1974 na akahudhuria shule ya Usimamizi katikla jiji kuu la NewYork. Tangu mwaka wa 1970 hadi 1981, Larry alifanya kazi katika shirika la kimataifa, makaazi yake yakiwa Uingereza na Uropa. Katika mwaka wa 1982, alikuwa mwanzilishi na pia rais na Mkuu wa kampuni ya kibinafsi ya uwekezaji. Wakati mmoja alipokuwa safarini ya kuelekea Seoul, Korea, alikutana na Daktari Billy Kim, kiongozi mashuhuri wa kikristo aliyekuwa mchungaji wa kanisa la Kibaptisti lililo na washirika 16,000 kule Suwon Nchini Korea. Wakati huo Daktari Kim alikuwa Rais wa kituo cha utangazaji cha Far East nchini Korea. Akichochewa na mkutano huo na kuongozwa na Roho mtakatifu, Larry alijitoa waziwazi kushiriki Yesu Kristu kote ulimwenguni na watu wa kila imani popote waishipo kwa njia itakayoeleweka. Ilikuwa ni mwaka wa 2004 wakati huduma ya Christ To The World ilianzishwa. Maono ya huduma ya Christ To The World ni kuongoza watu kumjua Mungu mmoja wa kweli na kupata ufahamu wa wokovu wa Yesu: Na kumuamini Yesu kama Mwokozi na Bwana. CTTW hutoa rasilimali inayoangazia neno la Mungu. Rasilimali hizo zinaegemea upande wa, kabla ya uinjilisti, uinjilisti na uanafunzi. Rasilimali hizi zote ndizo njia za kimsingi zinazotumiwa kuhadithia kupitia kwa njia ya kuigiza ili kuwasilisha ukweli wa maandiko. Huduma ya Christ to the World inatumia vyombo vya habari kueneza hadithi kutoka kwa bibilia katika nchi tofauti kote ulimwenguni.  

Email Sign-up

Sign up for the TWR360 Newsletter

Access updates, news, Biblical teaching and inspirational messages from powerful Christian voices.

Thank you for signing up to receive updates from TWR360.

Required information missing