Sherehe
-
Zaburi 121:1-4
Close
Moto Mkubwa
Katika programu thelathini na moja, moto mkubwa wanaoshindwa kuzuia inafikia pahala panapoitwa mwganza. Wato wote wa kijiji, wachanga, wazee na hata wagonjwa wanakuja pamoja kupigana na moto hili. Pamoja, wanajifunza umuhimu wa kuishi kama jamii moja.
Matumaini Yapatikana
Katika kipindi cha thelathini, Bahati na Riziki wanampata mtoto alieachwa kando ya nyumba yao. Pamoja wanamridhisha Nyanya aweke mtoto huyo. Watu wengi kijijini wanamkata mtoto huyo wakidhani kuwa ana virusi vya ukimwi.Bahati, Riziki na Nyanya, wanajifunza kuhusu huruma, matumaini na haki.
Zawadi Tofauti
Katika kipindi cha ishirini na tisa, Bahati na Riziki wanajitolea kusaidia katika hospitali siku nzima. Riziki anaonyesha huruma kwa kugusia hasia za wagonjwa hawa wa virusi vya ukimwi na Bahati anasaidia wagonjwa hawa na mahitaji zao za kimwili.wote wanajifunza kuwa kupeana huduma ni kitu cha maana sana.
Joseph amjua Yesu
Katika kipindi cha ishirini na nane, Mjomba Baba anatuma pesa ya kununua baiskeli mpya ya Bahati na Riziki. Watoto hawa wanaitumia kuwapa msaada familia waliokabiliwa na virusi vya ukimwi.
Nyumba la Jua
Katika kipindi cha ishirini na saba, Kikundi cha Vijana kutoka kanisani wanatembelea watu wanaoishi na virusi vya ukimwi hospitalini na kujifunza kuhusu huruma.
Mamba Nyeusi
Katika kipindi cha ishirini na sita, Daktari Baraza hurudi na kuzungumzia darasa la Bahati kuhusu virusi vya ukimwi. Wanafunzi wanajifunza kuhusu kinga na jinsi ya kuwalinda walioambukizwa ugonjwa huu.
Jitu
Katika kipindi cha ishirini na tano, wakati jirani wa Bahati anapokufa kutokana na virusi vya virusi vya ukimwi. Bahati anachukua hatua wa kumwalika daktari aje kuzungumzia darasa lake kuhusu virusi vya ukimwi.
Bahati Asema Hapana
Katika kipindi cha ishirini na nne, Pendo anajaribu kumkazia Bahati afanye mapenzi na yeye. Bahati anazungumza kuhusu hili jambo na Juma na elder Baraka na kuamua kukataa.
Tumi Asema Hapana
Katika kipindi cha ishirini na tatu, Tumi anakubali kwenda kwa nyumba ya Chokoza. Chokoza anajaribu kumkazia wafanye mapenzi lakini Tumi anatoroka. Wasichana kutoka shule ya Tumi wanamuona akitoka kwa Chokozana hili ninamuharibia jina.
Uaminifu
Katika kipindi cha ishirini na mbili, Toot Toot anarudi kijiji na Nyanya yake Karena. Karena anamuelezea Nyanya majaribu alionayo ya kuwa muongo katika ndoa. Pamoja, Nyanya na bwana wanarekebisha ndoa yao, wanapimwa virusi vya ukimwi na kuamua kuwa waaminifu katika ndoa.