Agano la Kale
-
Kitabu 1: Adamu na Hawa
Je, unaweza fikiria tu ingekuwaje kuona dunia vile Mungu alivyoiumba ama kutembea na Adamu na Hawa katika shamba la Edeni? Hebu tuanze kutoka mwanzo, katika kitabu cha Mwanzo. Mungu aliuumba ulimwengu, na kila kilicho ndani yake, ikiwa ni pamoja na Adamu Na Hawa. Lakini punde tu adui angetokea -
Kitabu 2: Nuhu
Ushawahi jiuliza ingekuwaje kuweza kumsaidia Nuhu kujenga mashua kuu, ama kusafiri naye na wanyama wote hao walionuka na kupiga makelele? Hii ni hadithi ya Mungu akiokoa familia iliyompenda wakati mafuriko makuu yalipotokea. Nuhu alijua ya kwamba itakuwa vigumu kumtii katika dunia iliyojaa watu waliofuata njia zao binafsi. Lakini Nuhu alijifundisha kumuamini Mungu na kumtii hata ilipokuwa ngumu kwake- na wewe pia unaweza fanya vivyo hivyo -
Kitabu 3: Ibrahimu
Ingekuwaje kusafiri na Ibrahimu hadi kwa nchi ya ahadi ambayo alikuwa hajaiona, ama kusherehekea ahadi za mungu wakati Isaka alipozaliwa? Mungu alimpa ahadi Ibrahimu, na hakuacha chochote kiingilie na ahadi hizo kutimia. Hata wakati Ibrahimu alikuwa na shauku na kufanya makosa, Mungu alikuwa anampenda na mwenye msamaha. -
Kitabu 4: Isaka na Rebeka
Ingekuwaje kuweza kumwona Isaka, Rebeka, Yakobo na Esau? Mungu alitenda mipango yake kupitia familia hii spesheli. Isaka na Rebeka waligundua ya kwamba Mungu alikuwa na mipango kuu kwa familia yao, na ilikuwa tofauti kuliko chochote walichotarajia! Hebu tujifunze nao kwanini ni muhimu kuamini mipango ya Mungu, na si yetu binafsi -
Kitabu 5: Yakobo
Je, ulijua ya kwamba watu kwenye Biblia walikuwa na shida katika familia zao kama tunazokuwa nazo siku hizi? Mungu alikuwa na Yakobo wakati ambapo hakuna mtu angekuwa naye, hata baada ya shida nyingi za familia. Yakobo alisafiri pekeyake, akiwa na bakora yake tu, kwa nchi ya mbali. Hebu tufuatilie safari yake na tujue kuhusu mambo aliyopitia njiani na lini alipofika katika nchi ile ya mbali. Mungu angepeleka ahadi zake kwa dunia nzima kupitia watoto tutakaopatana nao katika hadithi ya Yakobo -
Kitabu 6: Yusufu na ndoto zake
Je, ushawahi kuwaza ingekuwaje kuona koti la Yusufu la rangi nyingi ya upinde au kutembea katika bustani za Misri? Hii hapa ni hadithi ya kijana mdogo ambaye ndoto zake zilikuja kuwa kweli kwa njia ya kushangaza! Mungu anaweza geuza jambo baya likawa jambo zuri, na kutusaidia kusamehe waliotuumiza. Mugnu alikuwa na Yusufu, na Mungu ako nasi pia. -
Kitabu 7: Musa mtoto aliyeokolewa
Ingekuwaje kuweza kumsaidia Musa akiwa mchanga kutoka kwa kikapu katika mto, au kutembea naye jangwani? Mungu ana mipango ya kuokoa watu wake huko Misri, na alimtayarisha Musa kwa kazi hiyo kwa njia ya ajabu. Hkuna linaloweza kuzuia mipango ya Mungu, na anajali wakati watu wake wanateseka. Mungu ana mipango kuu kwa Musa, na pia Mungu ana mipango kuu kwetu ! -
Kitabu 8: Musa na kuhepa kwake
Je, ushawahi kujiuliza ingekuwaje kutembea katika Mto wa Nile huko Misri na Musa na kuona miujiza ya Mungu? Ama ingekuwaje kumuona Mungu akitenganisha maji ya Bahari ya Shama na kuona watu wote wa Mungu wahihepa utumwa na kuwa huru? Hii hapa ndiyo hadithi akiwaweka huru kutoka kwa mateso. Mungu ana nguvu kuu na alitenda miujiza makuu, na hata kama watu wake walikuwa watumwa kwa muda, Mungu ana mipango mema kuwaleta nyumbani. -
Kitabu 10: Musa na Nyumba ya Mungu
Musa na Nyumba ya Mungu, please add the following summary: Je? Ushawaji kufikiria ingelikuwaje kuishi katika siku za Bibilia? Kutembea na wana wa Israeli jangwani, kukutana na wanaume na wanawake na watoto waliosikia kuhusu amri za Mungu kwa mara ya kwanza? Kuzigusa pazia maridadi za hema la kukutania na kumwabudu Mungu, jinsi walivyofanya zamani? Hizi ni hadithi hai za Bibilia na zinasimulia kuhusu waisraeli jinsi walivyomuabudu Mungu aliyewaumba, kuwapenda na kuwaokoa.Tunaweza kumwabudu Mungu papa hapa tulipo naye ametuonyesha njia ya kupokea msamaha wa dhambi na ondoleo la aibu pia. -
Kitabu 17: Samsoni Mharibifu
Yaweza kuwaje kutazama jinsi Mungu alivyowalinda watu wake na kuwapiga maadui wa Waisraeli kupitia kwa viongozi,mahakimu na wafalme? Hii ni hadithi ya mwa zo wa shujaa mkubwa wa Bibilia aitwaye Samsoni. Hata ingawa Samsoni alifanya baadhi ya maamuzi mabaya,Mungu alikuwa na mipango mikubwa katika Maisha yake na alikuwa anaenda kumtumia kuwaokoa watu wa Israeli.Mungu angali anawainua madhujaa na viongozi leo,na ana mpango wa kupendeza maishani mwako pia. -
Kitabu 20: Yona
Yona, please add the following summary: Je umewahi kufikiri jinsi ingekuwa kukutana na manabii mashuhuri ambao walipata jumbe moja kwa moja kutoka kwa Mungu,na watu ambao walipewa jumbe hizi za kufurahisha? Nabii Yona aliishia kwa meli iliyokumbwa na kimbunga na Mungu alimwokoa yeye na watu wa Nineve katika njia za ajabu,hata ingawa hawakustahili upendo na huruma ya Mungu. Mungu anakualika uachane na dhambi zako na tabia ya kutotii,na ana hamu ya kutusamehe na atatusaidia tu ikiwa tutamwanini.