Wakristo wa Yerusalemu walionea shauku wakristo wa korintho kwa upendo na ukarimu wao. Waliowaombea na kumshukuru Mungu. Na hiyo ndiyo ahadi ya utoaji kwa ukarimu ukifanya hicyo watamtamani na hata kutilia maanani Imani yao katika Kristo bwana na mwokozi wetu. Mungu ndiye anayetuahidi hayo.
Kwanini ibrahimu alijulikana sana katika historia ya biblia? Jibu ni kwamba ibrahimu alikuwa mtu wa vitendo na mtu wa Imani na ndiye baba yetu. Lakini mtume Paulo amwonaje ibrahimu?
Ni vyema na Baraka kuu kuweka na kupalilia Imani yako kwa maombi na kujitwalia kanuni na ahadi za mungu kuliko kiburi na kujigamba kwako anapojigamba mtu huwa amesahau ule upendo wa kwanza kanisa al epheso lilikuwa katika hali hiyo hata mungu akamwamuru yohana kuwakumbusha ya kwamba kanisa lile lilikuwa lieacha upendo wa kwanza na lilipaswa kutubu na kuungama na kuurejesha uhusiano mwema na mungu.