Muhtasari: Ruthu

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Ruthu, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Katika Ruthu, familia moja ya Waisraeli inakabiliwa na msiba wa wanafamilia, na Mungu anatumia uaminifu wa mwanamke asiye Mwisraeli kuleta marejesho katika familia ya Daudi. #BibleProject #Biblia #Ruthu

Muhtasari: Waamuzi

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Waamuzi, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Katika Waamuzi, Waisraeli wanamuasi Mungu na wanakabiliwa na matokeo ya uasi wao. Mungu anateua waamuzi katika vipindi vya uasi, toba, na marejesho. #BibleProject #Biblia #Waamuzi

Muhtasari: Yoshua

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Yoshua, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Baada ya kifo cha Musa, Yoshua anaongoza taifa la Israeli na wanakaa katika nchi ya ahadi inayomilikiwa na Wakanaani kwa sasa. #BibleProject #Biblia #Yoshua

Muhtasari: Kumbukumbu la Torati

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Kumbukumbu la Torati, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Katika Kumbukumbu la Torati, Musa anatoa maneno ya mwisho ya hekima na onyo kabla Waisraeli hawajaingia katika nchi ya ahadi, akiwapa changamoto wawe waaminifu kwa Mungu. #BibleProject #Biblia #KumbukumbulaTorati

Upendo wa Agape

Neno “upendo” ni mojawapo ya maneno mazito zaidi katika lugha yetu, kwa kuwa kimsingi hurejelea hisia zinazozaliwa ndani ya mtu. Katika Agano Jipya, “upendo” au "Agape" humaanisha njia ya kuwatendea watu iliyofafanuliwa na Yesu mwenyewe: kutafuta ustawi wa wengine bila kujali wataitika vipi au watakutendeaje wewe. #BibleProject #Biblia #Agape

Tumaini

Katika Biblia watu wenye tumaini ni tofauti sana na watu wenye mtazamo chanya! Katika video hii, tutajadili jinsi tumaini la Biblia linavyoainisha tabia ya Mungu peke yake kama msingi wa kuamini kuwa siku zijazo zitakuwa bora kuliko za sasa. #BibleProject #Biblia #Tumaini

Muhtasari: Mambo ya Walawi

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Mambo ya Walawi, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Katika kitabu cha Mambo ya Walawi, Mungu mtakatifu wa Israeli anawaalika Waisraeli kuishi katika uwepo wake licha ya dhambi zao, kupitia msururu wa ibada na taasisi takatifu. #BibleProject #Biblia #MamboYaWalawi

Furaha

Katika video hii, tutazungumzia aina ya kipekee ya furaha ambayo watu wa Mungu wameitwa kuwa nayo. Ni zaidi ya hisia ya furaha, kinyume na hapo ni uamuzi wa kuamini kuwa Mungu atatimiza ahadi zake. #BibleProject #Biblia #Furaha

Shalom - Amani

"Amani" ni neno la kawaida sana katika Kiswahili, linalomaanisha mambo tofauti kwa watu tofauti. Pia ni neno muhimu sana katika Biblia. Neno hili hurejelea hali ya kutokuwepo kwa migogoro. Lakini pia hurejelea uwepo wa kitu kingine. Katika video hii tutachunguza kwa ina maana ya msingi ya amani ya kibiblia, au Shalom na jinsi inavyofungamana na Yesu. #BibleProject #Biblia #Amani

Muhtasari: Kutoka 1-18

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Kutoka 1-18, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Katika kitabu cha Kutoka, Mungu anawaokoa Waisraeli kutoka utumwani katika nchi ya Misri na anakabiliana na uovu na udhalimu wa Farao. #BibleProject #Biblia #Kutoka

Muhtasari: Hesabu

Tazama video yetu ya muhtasari wa kitabu cha Hesabu, inayoelezea muundo wa fasihi ya kitabu hicho na mtiririko wake wa mawazo. Katika Kitabu cha Hesabu, Waisraeli wanasafiri nyikani wakielekea katika nchi aliyoahidiwa Abrahamu. Uasi wao wa mara kwa mara unakutana na hukumu na rehema ya Mungu. #BibleProject #Biblia #Hesabu Wahusika Katika Utayarishaji wa Video: Timu Ya Utayarishaji Wa Toleo La Kiswahili Tai Plus Dar es Salaam, Tanzania Toleo la Asili la Kiingereza na Utayarishaji Wake BibleProject Portland, Oregon, USA

sajili ya -barua pepe

Sign up for the TWR360 Newsletter

Access updates, news, Biblical teaching and inspirational messages from powerful Christian voices.

Ahsante kwa kujisajili ili kupata ujumbe kutoka TWR360Thank you for signing up to receive updates from TWR360.

Habari inayohitajika haipo