Barua za Agano Jipya: Muktadha wa Fasihi
Barua za Agano Jipya: Muktadha wa Kihistoria
Katika Agano Jipya, kuna barua 21 au nyaraka zilizoandikwa na viongozi wa Kikristo wa mwanzoni kwenda katika jumuiya za wafuasi wa Yesu zilizokuwa katika ulimwengu wa kale wa himaya ya Roma. Kusoma kwa hekima barua hizi kunahusisha kujifunza kuhusu muktadha wake wa kihistoria. Barua hizo ziliandikwa kwa akina nani, wapokea barua hizi waliishi wapi, na ni nini kilichochochea kutuma barua hiyo? Katika video hii, tunachunguza safu tofauti za muktadha wa kihistoria kwa kutumia barua hizi ili tuweze kuelewa vyema hekima zinazotoa leo hii. #bibleproject #Biblia #nameofvideo
Mifano ya Yesu
Yesu wa Nazareti alikuwa mtaalamu wa kuwasilisha simulizi, na mafundisho yake mengi yanayojulikana sana yalielezwa kama mifano. Lakini simulizi hizi zilibuniwa ili kufanya kazi kubwa zaidi tu ya kufundisha. Yesu alisema kwamba mifano hiyo ilibuniwa ili kufichua na kuficha ujumbe wake kuhusu kuwasili kwa Ufalme wa Mungu. Katika video hii, tunachunguza mada kuu katika mifano ya Yesu na kujiuliza kwa nini alitumia mifano kama njia kuu ya kufikisha ujumbe wake. #bibleproject #Biblia #nameofvideo
Injili
Agano Jipya lina vitabu vya wasifu wa Yesu wa Nazareti vinne na kwa pamoja huitwa Injili. Kila moja linaelezea simulizi hii kama tangazo la Habari Njema kwamba Yesu aliyesulubiwa na kufufuliwa ndiye mtawala wa kweli wa mataifa. Katika video hii tunachunguza kwa nini masimulizi haya yaliandikwa na jinsi unavyoweza kuyasoma kwa ufahamu mkubwa. #bibleproject #Biblia #nameofvideo
Sitiari katika Mashairi ya Kibiblia
Kuelewa jinsi sitiari zinavyotumiwa katika Biblia ni ujuzi muhimu wa kusoma mashairi ya kibiblia. Wakati wowote mtu anapoelezea kitu kimoja ili kuelezea kitu kingine, anatumia fikra za kifumbo, iwe anatambua au la. Sitiari zipo kila mahali katika Biblia na katika mazungumzo yetu ya kila siku. Katika video hii, tutachunguza kipengele hiki muhimu cha lugha ya kibiblia. #bibleproject #Biblia #nameofvideo Wahusika Katika Utayarishaji wa Video: Timu Ya Utayarishaji Wa Toleo La Kiswahili Tai Plus Dar es Salaam, Tanzania Toleo la Asili la Kiingereza na Utayarishaji Wake BibleProject Portland, Oregon, USA
Ufundi ya Mashairi ya Kibiblia
Je, unajua kwamba theluthi moja ya Biblia ni mashairi ya Israeli ya kale? Mashairi ni sanaa tajiri inayotumika na binadamu kufanya mawasiliano, lakini mara nyingi ni vigumu kuelewa mashairi. Katika video hii, tutachunguza sifa za kipekee za mashairi ya kibiblia ili uweze kugundua uzuri na nguvu zake mwenyewe. #bibleproject #Biblia #nameofvideo
Mitindo ya Fasihi katika Biblia
Sehemu ya tatu inaonyesha jinsi kusoma Biblia kwa hekima kunatuhitaji kujifunza kuhusu mitindo ya fasihi ya kale iliyotumiwa na waandishi wa kibiblia. Waandishi hawa walielezea mawazo na madai yao kwa aina tofauti za fasihi, na video hii itachunguza kwa nini ni muhimu kutambua aina hizo ili tuweze kusikia ujumbe wao kwa mujibu wa walichokusudia wao. #bibleproject #Biblia #nameofvideo
Simulizi ya Biblia
Video hii inatoa muhtasari wa simulizi ya Biblia kama mfululizo wa maamuzi makubwa na ya muhimu. Binadamu huendelea kujifafanulia upya mema na mabaya, jambo linaloishia katika maumivu na kuishia uhamishoni. Kisha anafuata Yesu, anayechukua njia tofauti inayofungua njia ya uumbaji mpya. #bibleproject #Biblia #nameofvideo
Biblia ni nini?
Hii ni sehemu ya kwanza ya mfululizo unaoendelea unaochunguza chanzo, maudhui, na kusudi la Biblia. Hapa utatambulishwa kwenye historia fupi ya jinsi Biblia ilivyoumbwa na aina tofauti za Biblia katika mila za Kikristo za Katoliki, Kiorthodoksi, na Kiprotestanti.#bibleproject #Biblia #Biblianinini
Injili ya Luka Sura ya 9-19
Sehemu ya tatu inaangazia sehemu ya katikati ya Injili ya Luka. Yesu anaendelea na tangazo lake tatanishi la habari njema kwa maskini akiwa kwenye safari ndefu ya kuelekea Yerusalemu, tangazo linalochochea mgogoro na viongozi wa dini. Mgogoro huu unatengeneza mazingira ya kusimulia simulizi maarufu ya Mwana mpotevu. Wahusika Katika Utayarishaji wa Video: Timu Ya Utayarishaji Wa Toleo La Kiswahili: Tai Plus na Eternal Entertainment, Dar es Salaam, Tanzania Toleo la Asili la Kiingereza na Utayarishaji Wake: BibleProject, Portland, Oregon, USA #BibleProject #Biblia #Luka
Injili ya Luka Sura ya 3-9
Ya pili katika Mfululizo wa sehemu tano kuhusu Injili ya Luka. Tunamwona Yesu akianzinsha utume wake wa habari njema kwa maskini na jinsi alivyowaleta watu wa aina mbalimbali kuishi pamoja kwa amani. Wahusika Katika Utayarishaji wa Video: Timu Ya Utayarishaji Wa Toleo La Kiswahili: Tai Plus na Eternal Entertainment, Dar es Salaam, Tanzania Toleo la Asili la Kiingereza na Utayarishaji Wake: BibleProject, Portland, Oregon, USA #BibleProject #Biblia #Luka